Aliyenusurika meno ya Papa kurejea A.Kusini

Haki miliki ya picha epa
Image caption Fanning anasema kuwa atarejea Afrika Kusini

Muogeleaji wa kuteleza kwenye mawimbi raia wa Australia aliyenusurika kung'atwa na papa Mick Fanning akishiriki mashindano ya kimataifa amesema kuwa atarejea kwenye mchezo huo.

Fanning amefanya maamuzi hayo magumu ya kurejea tena kwenye mchezo wake huo siku chache tu baada ya kuokolewa kutoka baharini alipovamiwa na papa wakati wa mashindano ya kimataifa huko Afrika Kusini.

Mtelezaji huyo mawimbini amewaeleza waandishi habari hofu kubwa iliyomkumba alipoona anafuatwa na papa wakati aliporejea nyumbani kwao mjini Sydney.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Aliwashukuru washindani wenza waliomuokoa

Mick Fanning alianza kwa kumshukuru mshindani wenzake katika mchezo huo wa majini Julian Wilson ambaye aliogolea mbio mbio kwenda kumsaidia alipomuona akipambana na papa huyo. Na ingawa lilikuwa ni swala la kunusurika kutoka tundu ya sindano,

Aliuvunja ukungu wa tafakhari na hisia nzito zilizodhihirika katika mktano huo na wanahabari kwa ucheshi,,,

je una ujumbe gani kwa papa huyo ? aliuliza mwandishi

Haki miliki ya picha epa
Image caption Fanning ''ningemwambia papa asante kwa kutonila''.

Nae Mick akajibu kwa bashasha,

''ningemwambia papa asante kwa kutonila''.

Video zimekuwa zikisambaa mtandaoni zikimuonesha Mick alivyompiga Papa huyo ngumi na kifaa chake alichokuwa akikitumia kuogelea hadi akapata fursa kuogelea kasi kwenda kwenye boti lililokuja kumuokoa . ''Naamini wenzangu walikuwa wakinifuatilia nikiwa majini ndio haraka wakaja kunisaidia kwani kunusurika kutoka hatari ya kumezwa na jisamamaki hilo jikubwa pasi na hata mkwaruzo mwembamba , hiyo kweli ni miujiza ," Mick amenukuliwa kusema.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Mick anasema bado hajaelewa ilikuaje hasa papa huyo alikuwa akimfuata fuata lakini katu hawakumuona.

Mick anasema bado hajaelewa ilikuaje hasa papa huyo alikuwa akimfuata fuata lakini katu hawakumuona.

Na pia hakuelewa kama alivyokuwa akimpiga alihisi ni kama anapigwa makonde ya kitoto au alihisi vipi?

Kwao nyumbani Australia maelfu ya kilomita nyingi kutoka pwani hiyo ya J BAY huko Afrika kusini mamake Mick, alikuwa akiona tukio hilo moja kwa moja kupitia kwa runinga yake sebuleni kwake.

Alieleza vyombo vya hahari jinsi alivyoshtuka na kurukia TV hiyo kama na mikono yake ikijaribu kumuokoa mwanawe lakini bila shaka alikuwa akigusa tu kioo cha runinga!

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mamake Mick, alikuwa akiona tukio hilo moja kwa moja kupitia kwa runinga yake sebuleni kwake.

Bila shaka hata nawe ulipo unaweza kuhisi afueni aliyopata alipomwona Mick akifanikiwa kumkwepa Papa huyo.

Washindani wenzake waliomuokoa nao walisema jinsi ilivyokuwa katika hali ya mshikeshike huku wakiomba Mungu wafanikiwe kumnusuru mwenzao kutoka kwa meno ya papa.

Sasa kinachowashangaza wengi ni kwamba Mick anasema japo anafunga safari ya kwenda kwao Australia bado atarudi Afrika Kusini kuogelea !

Anasema ataendelea kushiriki mashindano hayo ya kuteleza baharini licha ya tukio hilo, tena katika pwani hiyo hiyo ya J B Afrika Kusini.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mick anasema japo anafunga safari ya kwenda kwao Australia bado atarudi Afrika Kusini kuogelea !

Sabau zake- asema mchezo huo wa majini ndio humpa amani ya nafsi.

Ningepewa nafasi ya kumshauri ningemwambia pengine ajaribu kuzuru pwani zetu za Afrika Mashariki - ambako siku hizi Papa ambae ni kitoweo maarufu kwa wakazi wa mwambao huo ameadimika sana.

Huko ataogelea na kuteleza kwenye mawimbi bila kuvurugiwa amani ya nafsi na papa.