Usajili wa kielektroniki Tanzania umeanza

Image caption Usajili wa kielektroniki Tanzania umeanza

Leo imeingia siku ya pili kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujiandikisha katika daftari la kupiga kura kwa kutumia mfumo wa kieletroniki maarufu kama BVR.

Image caption Wakazi wapatao milioni tano ambao wana sifa ya kupiga kura wanalengwa

Katika zoezi hili ambalo linatarajiwa kudumu kwa siku kumi, tume ya uchaguzi ya taifa inatarajia kusajili wakazi wapatao milioni tano ambao wana sifa ya kupiga kura.

Image caption Zoezi hili linatarajiwa kudumu kwa siku kumi

Hata hivyo, wakati zoezi hilo likiendelea, tayari linaonekana kuwa kero miongoni mwa wakazi.

Image caption Vituo vingi vinadaiwa kucheleweshwa

Katika baadhi ya vituo ambao inaarifiwa kuwepo kwa ucheleweshwaji huku katika maeneo mengine kukiwa na mashine chache za uandikishaji.

Image caption Mashine zinadaiwa kuwa chache

Je umejiandikisha kupiga kura katika mfumo huo mpya wa kielektroniki?

Tusimulie yaliyokusibu