Burundi kunyimwa misaada na Umoja Ulaya

Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Muungano wa Ulaya EU umeanza kikao maalum kujadili uwezekano wa kukata msaada wake nchini Burundi.

Inakisiwa kuwa fedha kutoka muungano huo unafikia zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya Burundi ya kila mwaka.

Mkuu wa masuala ya kigeni wa Muungano wa EU Federica Mogherini, ameelezea wasiwasi wake juu ya ghasia zilizototokea nchini humo kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais, na ametilia shaka iwapo serikali itakayoundwa baada ya uchagzui huo itakuwa wakilishi ya taifa nzima.

Upande wa uchaguzi ulsusia kura hiyo iliyofanywa siku ya Jumanne. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Ijumaa hii.

Uamuzi wa Rais Pierre Nkurunzinza kuwania urais kwa muhula wa tatu umetajwa kwenda kinyume na mkataba waliosaini mjini Arusha miaka kumi na tano iliyopita, ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mingi.