Obama:Kutodhibiti silaha kumenisononesha

Image caption Rais Barack Obama wa Marekani

Katika mahojiano maaluma na BBC , Rais wa Marekani Barack Obama amesema kushindwa kudhibiti silaha nchini mwake ni jambo lililomsononesha katika utawala wake.

Amesema Marekani ni nchi pekee iliyoendelea ambayo haina sheria ya kutosha kuhusu usalama wa silaha, hata wakati huu ambapo kumekuwa na marudio ya matukio ya mauaji.

Obama amesema magaidi wameua chini ya wamarekani mia moja tangu shambulio la kigaidi la Septemba 11, lakini waliouawa kwa matukio ya kutumia silaha ni makumi kwa maelfu katika kipindi hicho.

Rais Obama alijaribu kusukuma mbele sheria ya udhibiti wa silaha baada ya tukio la mauaji kwenye shule moja inayojulikana kwa jina la Sandy Hook School mwaka 2012, lakini sheria hiyo ya kubana matumizi ya silaha ilikataliwa na bunge la Congress.