Obama kufungua mkutano wa biashara Kenya

Haki miliki ya picha AFP GETTY
Image caption rais Obama

Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa kufungua mkutano mkubwa wa kibiashara katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kipekee nchini Kenya.

Amepongeza kile alichokitaja kuwa maendeleo ya kibiashara na anatarajiwa kusisitiza kuhusu vita dhidi ya ufisadi nchini.

Atazuru eneo la kumbukumbu za bomu katika eneo la uliokuwa ubalozi wa Marekani kabla ya mazungumzo kuhusu usalama na rais Uhuru Kenyatta.

Image caption Rais Obama akijumuika na familia yake mda mfupi alipowasili Kenya.

Rais Obama aliwasili mjini Nairobi siku ya ijumaa kwa ziara yake ya kwanza akiwa rais nyumbani kwa babaake huko.

Ziara hiyo imetajwa kuwa ya kurudi nyumbani na vyombo vya habari na makundi ya raia walioushangilia msafara wa Obama wakati ulipokuwa ukitoka katika uwanja wa ndege wa Jomo kenyatta Jijini Nairobi.

Siku ya jumamosi ,rais huyo wa Marekani ataongoza ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kibiashara ,baadaye rais Obama atazuru eneo la kumbukumbu katika uliokuwa ubalozi wa Marekani.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Obama

Zaidi ya watu 200 waliuawa ikiwemo raia 12 wa Marekani pamoja na wafanyikazi 34 wa ubalozi huo wakati wa shambulizi hilo lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Alqaeda.

Shambulizi jengine kama hilo lilifanyika sambamba na lile la Nairobi la jijini Dar-es-Salaam Tanzania ambapo takriban watu 11 waliuawa na wengine 70 wakijeruhiwa.

Baadaye rais Obama anatarajiwa kufanya mazungumzo ya kibiashara na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Image caption Rais Obama

Mwandishi wa BBC Karen Allen anasema kuwa ni maswala ya usalama na mikakati ya kukabiliana na ugaidi ndio yatakayotawala mazungumzo hayo.

Kenya imelengwa na wapiganaji wa Alshabaab ambao wamewaua takriban watu 67 katika shambulizi lililotekelezwa katika duka la West Gate mnamo mwaka 2013.

Kundi hilo pia lilitekeleza shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa,kazkazini mwa Kenya mapema mwaka huu ambapo liliwaua watu 148.