Mbunge auawa Somalia

Image caption Rais wa Somalia Sheikh Hassan Mahmoud amesema kuwa wapiganajai wa Al Shabab wamempiga risasi mbunge

Rais wa Somalia Sheikh Hassan Mahmoud amesema kuwa wapiganajai wa Al Shabab wamemuua mbunge mmoja saa chache baada ya Rais wa Marekani Barack Obama kusema kuwa uwezo wa kundi hilo umedhoofishwa.

Eneo la kaskazini mwa nchi hiyo limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na wapiganaji wa Boko Haram kutoka Nigeria.

Karibu saa tatu unusu usiku saa za Afrika Mashariki idadi iliyokuwa imethibitishwa ya waliofariki ni watu 14.

Washambuliaji hao walifyatulia risasi gari la mbunge Abdulahi Hussein Mohamud alipokuwa akisafiri katika wilaya ya kusini ya mji mkuu wa Mogadishu na kumuua papo hapo pamoja na walinzi wake wawili na dereva.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alshabab inapigania kuipindua serikali ya Somalia

Rais Hassan Sheik Mohamud amesema alighadhabishwa na shamabulizi hilo,ikiwa la hivi punde zaidi kuwalenga wabunge wa Somalia.

Alisema kuwa licha ya mauaji ya mbunge huyo serikali yake itaendelea kupambana na ugaidi.

Alshababu imesema kuwa wapiganaji ndio waliofanya shambulizi hilo na kuonya kuwa wataendelea kuwalenga wabunge.

Alshabab wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kujitolea mhanga na kuwalenga viongozi serikalini.

Balozi wa Umoja wa mataifa huko Somalia Nicholas Kay amesema mauaji hayo ni kitendo cha kikatili.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Huyu sio mbunge wa kwanza kuuawa na wapiganaji wa Al Shabaab

Alshabab inapigania kuipindua serikali ya Somalia inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na kulindwa na vikosi vya wanajeshi 22,000-wa muungano wa Umoja wa Afrika(AMISOM).

Shambulio hilo limefanyika wakati Obama yuko katika nchi jirani ya Kenya ambako alisifu jitihada za AMISOM ambaye alisema kuwa japokuwa wapiganaji hao wamethibitiwa bado kuna haja ya kuboresha usalama ili kulizima kabisa.

Vikosi vya serikali vikisaidiwa na vile vya umoja wa Afrika vilifanya mashambilizi kusini mwa Somalia katika opareheni inayohusisha majeshi ya Kenya na Ethiopia.