Aliyemuua simba maarufu Zimbabwe asakwa

Haki miliki ya picha Paula French
Image caption Zimbabwe

Msako mkali unaendelea nchini Zimbabwe dhidi ya mwindaji haramu aliyemuua mmoja kati ya simba maarufu nchini humo .

Mtu huyo anaaminiwa kumlipa mmoja wa walinzi wa wanyamapori katika mbuga ya wanyamapori ya Hwange zaidi ya kilomita elfu hamsini kumuua simba huyo 'Cecil the lion' mapema mwezi huu .

Mmoja wa wanaharakati wa wanyamapori Johnny Rodrigues ameiambia BBC kuwa mnyama huyo alidungwa na mkuki na pia kupigwa risasi , kabla ya kukatwa kichwa na kutolewa ngozi .

Simba huyo mwenye umri wa miaka 13 alikua kivutio maarufu katika mbuga hiyo.

Amekua akivalia rangi ya kutambuliwa na setilait aliyovalishwa na watafiti wa chuo kikuu cha Oxford cha Uingereza.

Zimbabwe imekuwa na changamoto ya kukabiliana na wawindaji haramu wa wanyamapori