Mtambo wa simu bandia za iphone wavamiwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Iphone

Kampuni iliyodaiwa kutengeneza simu bandia 41,000 aina ya Iphones kutoka kampuni ya Apple imevamiwa huko Uchina na watu 9 kukamatwa.

Oparesheni hiyo ilishirikisha mamia ya wafanyikazi waliokuwa wakiandaa vipuri vya simu vilivyotumika kama simu mpya aina ya iphone tayari kuuzwa nje,huku simu hizo bandia zikizalisha kitita cha dola miloni 19.

Kampuni hiyo iligunduliwa tarehe 14 mwezi Mei lakini ikabainika katika mitandao ya kijamii na ofisi ya usalama ya umma Beijing siku ya jummapili.

Oparesheni hiyo ilianzishwa mwezi wa januari.

Uchunguzi huo uliongozwa na kundi la mke na mumewe kaskazini mwa mji mkuu wa Uchina, kulingana na mamlaka ya Beijing.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kampuni hiyo ilikuwa imetengeza simu bandia 41,000.

Walisema kuwa walidokezewa na mamlaka ya Marekani ambayo ilinasa simu hizo bandia .

Ripoti hiyo inajiri wakati kuna msako wa bidhaa bandia unaotekelezwa na Uchina huku mamlaka hiyo ikiyashinikza makampuni kuweka nembo za ubora wa biadha.

Uchina pia imekubali kufanya kazi na mamlaka ya Marekani kupunguza kuwepo kwa bidhaa bandia zinazotoka nchi hizo mbili.