Obama awaonya viongozi wa Afrika

Haki miliki ya picha
Image caption Obama

Rais wa Marekani Barrack Obama ameonya kuwa bara la Afrika halitapiga hatua zozote za kimaendeleo iwapo viongozi wake watasalia madarakani hata baada ya wakati wao kuisha.

Vilevile Obama ametaka viongozi kukabiliana na swala la ufisadi akisema limechukua fedha nyingi za maedeleo.

Jana jioni rais Obama alikutana na viongozi wa nchi za mashariki na pembe ya Afrika IGAD, kuzungumzia usalama hasa katika taifa changa zaidi duniani la Sudan kusini.

Obama ni rais wa kwanza wa Marekani kutoa hotuba kwa wanachama 54 wa umoja huo ,huku swala la usalama na vita dhidi ya ugaidi ikiwa ni miongoni mwa ajenda zake kuu.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Obama

Siku ya jumatatu rais Obama aliipongeza Ethiopia kama mshirika mkuu katika kukabilana na magaidi.

Amesema kuwa Ethiopia imechangia pakubwa katika kudhoofisha uwezo wa kundi la kigaidi la Alshabaab nchini Somalia.

Rais huyo wa Marekani alikuwa akizungumza baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakati wa ziara ya kwanza ya kiongozi wa Marekani katika taifa hilo la Afrika mashariki.

Pia alitoa wito kwa Hailemariam kuimarisha rekodi ya haki za binaadamu na utawala bora.