Isreal yapinga ripoti ya AI

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Israel

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Amnesty International linasema kuwa, kuna ushahidi wa kutosha kuwa, Israeli ilitekeleza uhalifu wa kivita pale ilipojibu shambulio la kutekwa nyara kwa askari wake mmoja mwaka jana wakati wa mzozo huko Gaza.

Jeshi la Israeli lilitekeleza kile ambacho ripoti ya Amnesty imeelezea kama matumizi ya nguvu ya silaha.

Shirika hilo linasema kwamba mizinga ilishambulia kwa kasi na bila ya kuchagua ni wapi inarushwa hasa kulikokuwa na idadi kubwa ya watu siku tatu mfululizo

Zaidi ya Wapalestina 135 waliuauwa.

Israeli imeikana ripoti hiyo, huku ikisema inaegemea upande mmoja na kwamba mtindo mbaya ulitumika kuiandaa.