HDP:Uturuki inapinga eneo la Kurdistan

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wafusi wa chama cha kikurdi nchini Uturuki PKK

Eneo salama linalobuniwa na Uturuki pamoja na Marekani ni jaribio la Ankara kuwazuia wakurdi kuanzisha eneo lao kulingana na kiongozi wa chama cha Kikurdi nchini Uturuki.

Kiongozi huyo wa HDP Selahatin Dermitas amesema kuwa oparesheni ya Uturuki dhidi ya wapiganaji wa Islamic State mpakani ni njama ya kuwalenga waasi wa Kikurdi wa PKK.

Ameitaka Uturuki na PKK kurejelea mazungumzo ya amani.

Uturuki pia imeshambuliwa na wapiganaji wanaoshirikiana na IS ikiwemo shambulizi moja lililowaacha watu 32 wakiwa wamefariki katika mji wa mpakani wa Suruc wiki iliopita.

Uturuki inayachukulia makundi ya PKK na IS kama mashirika ya kigaidi.

Kwengine, Marekani imethibitisha kuwa inafanya mazungumzo na Ankara kuhusu oparesheni ya pamoja dhidi ya IS nchini Syria.