Uzinduzi wa Windows 10 ni mwanzo mpya

Haki miliki ya picha Microsoft
Image caption Windows 10

Programu ya Windows 10 imeadhimisha mwanzo mpya katika kompyuta za kibinafsi ,kulingana na mtendaji mkuu wa kampuni ya Microsoft .

Programu hiyo ilizinduliwa kimataifa siku ya Jumatano, na ni jaribio la kampuni hiyo kujaribu bahati yake katika sekta ya simu.

Windows 10 itatolewa bure kwa wateja wengi kama hatua ya kuboresha programu hiyo.

Haki miliki ya picha MICROSOFT
Image caption Windows 1 hadi 10

Hata hivyo makampuni yatalazimka kulipia toleo hilo jipya hivyo watengenezaji wa PC watahitajika kuiweka katika vifaa hivyo.

Wachambuzi wanasema mkakati huo umezinduliwa ili kuharakisha utumizi wake.

Alipofanya mazungumzo ya kipekee na BBC, Satya Nadella alisema ''programu ya windows 10 ni hatua kubwa kwetu sisi kama kampuni, na katika sekta nzima''.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Windows 10

Microsoft imekua mbioni kuizindua kwa muda wa wiki kadhaa zilizopita, hivyo si kila mtu atapata fursa hiyo ya kuboreshewa siku ya kuanzishwa kwake.