Cameron atakiwa asiwadhalilishe wahamiaji

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri mkuu Cameron akiwasili Vietnam

Waziri mkuu wa Uingereza ameibua utata, kwa kuwafananisha wahamiaji haramu wanaojaribu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza kama ''bumba la nyuki''.

Baraza linalowashughulikia wakimbizi Nchini Uingereza, limesema kuwa hiyo ni "Lugha ya kuwadunisha watu'' hususan maneno hayo yakitoka kinywani mwa kiongozi kama mwenye hadhi kubwa ''duniani".

''Ni lugha ya kutamausha''.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Cameron atakiwa asiwadhalilishe wahamiaji

Waziri huyo mkuu ambaye yuko ziarani Vietnam alikuwa akitoa maoni kuhusiana na purukushani katika mji wa Calais, nchini Ufaransa, ambapo mamia ya wahamiaji,

wanajaribu kwa usiku wa tatu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza wakitumia kivukio cha chini kwa chini.

Bwana Cameron amesema kuwa Uingereza haitakuwa ''mahala salama'' kwa wahamiaji wanaotokea mji huo wa Calais.

Image caption Wahamiaji wakiabiri magari ya uchukuzi ilikuingia Uingereza

Aidha bwana Cameron ameonya kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo kulinda mipaka ya Uingereza.

Afisa wa Umoja wa mataifa, Peter Sutherland, anawashutumu wanasiasa wa Uingereza kwa kushughulikia jambo hilo kwa matamshi ya ''chuki dhidi ya wageni'' na matumizi ya lugha ya kuwadhalalisha.