Aliyefadhili mabomu Mumbai amenyongwa

Haki miliki ya picha
Image caption Aliyefadhili mashambulizi Mumbai anyongwa

Mtu aliyepatikana na hatia ya kufadhili kifedha mlipuko wa bomu wa mwaka 1993 mjini Mumbai amenyongwa katika gereza moja magharibi mwa India.

Yaqub Memon amenyongwa baada ya ombi lake la mwisho la msamaha kukataliwa na mahakama kuu pamoja na rais wa India .

Kulikuwa na matukio ya mfululizo wa kabal ya kunyongwa kwa bwana Yakub mapema leo asubuhi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kundi la mawakili,wanasiasa na wachezaji filamu walimuandikia barua rais wa nchi hiyo wakimuomba ampe msamaha lakini alikataa

Mahakama kuu ilifungua milango yake usiku kwa ajili ya kuisikiza rufaa ya mwisho ya bwana Yakub,lakini rufaa yake ikakataliwa mbali kabla ya alfajiri na mapema.

Bwana Yakub alikuwa amepatikana na hatia kufadhili kwa pesa na vifaa washambuliaji waliotikisa mji wa Mumbai kwa kulipua mabomu kadhaa mjini humo katika msururu wa mashambulizi mwaka wa 1993.

Watu 250 walipoteza maisha yao, huku wengine wengi zaidi wakijeruhiwa.

Haki miliki ya picha
Image caption Maafisa wa kulinda usalama wameimarisha doria mjini humo

Maafisa wa kulinda usalama wameimarisha doria mjini humo ilikuzuia kutibuka kwa maandamano na makabiliano baina ya wafuasi wake na vyombo vya dola.

Katika kipindi cha juma moja iliyopita maoni yalitofautiana kuhusu huku hiyo ya kifo iliyokuwa ikimkabili.

Kundi la mawakili,wanasiasa na wachezaji filamu walimuandikia barua rais wa nchi hiyo wakimuomba ampe msamaha lakini alikataa.