Mtoto wa mwaka moja achomwa moto West Bank

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtoto wa mwaka moja achomwa moto West Bank

Mazishi ya mvulana mdogo mpalestina, ambaye aliuwawa katika kisa cha kutekekezwa moto nyumba kwao huko West Bank, yamefanyika.

Mtoto huyo wa miezi 18 alifariki baada ya nyumba yao iliyoko katika kijiji cha Duma kusini mwa mji wa Nablus, kuteketezwa kwa moto baada ya kumwagiwa petroli.

Wazazi wa mtoto huyo na kaka yake pia walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu ameyataja kama lilikua tendo la ugaidi.

Wakazi wa kijiji hicho wanasema waliofanya shambulizi hilo waliandika neno "kisasi" kwa kiyahudi kwenye ukuta na kuweka nyota ya Mfalme Daudi.

Mwaandishi wa kidiplomasia wa BBC mashariki ya kati anasema kuwa, shambulio hilo linafanyika wakati ambapo hali ya usalama ni tete kati ya Israeli na Palestina, huku hali ya taharuki ikitanda kati ya kundi moja la walowezi la wa mrengo wa kulia na serikali ya Israeli.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serikali ya Israeili imetaja mauaji hayo kuwa ya ''kigaidi''.

Kuna mgawanyiko mkubwa kuhusiana na ongezeko la majengo mapya ya masetla wa kiyahudi huko Hebron.

Serikali ya Palestina inalaumu Israeli kwa kuwapa walowezi wa kiyahudi ardhi yao kinyume na sheria.

Wenyeji wa kijiji hicho cha Duma wanasema waliotekeleza shambulizi hilo waliandika ''kisasi'' kwenye ukuta wa vifusi vya nyumba hiyo pamoja na ishara ya nyota ya daudi.