Mgogoro wa uongozi wakumba Taleban

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wapiganaji wa Taleban kutoka Pakistan

Msemaji wa baraza kuu la kundi la Taliban nchini Afghanistan ameimbia BBC kuwa hawakuombwa ushauri wakati wa uteuzi wa hivi majuzi wa kiongozi mpya kufuatia kifo cha mwanzilishi wake Mullar Omar.

Msemaji wake Mullah Abdul Manan Niazi anasema kuwa baraza hilo litafanya mkutano ili kumchagua kiongozi mpya.

Image caption Wapiganaji wa Taleban kutoka Afghanistan

Siku ya Alhamisi taarifa za Taliban zilisema kuwa Mullah Akhtar Mansour alikuwa amechaguliwa kuliongoza kundi hilo.

Baadhi ya wanachama wa Taliban wamewalaumu wanachama wengine nchini Pakistan kwa kuwalazimishia Mullah Mansour kama kiongozi wao.