Wapiganaji 260 wa kikurdi wauawa

Haki miliki ya picha na
Image caption Turkey

Shirika la habari la taifa la Uturuki, linasema kuwa wapiganaji wa Kikurd 260 wameuawa katika mashambulio ya ndege ya juma moja, dhidi ya kundi la PKK, lilopigwa marufuku.

Mashambulio hayo yamefanywa nchini Uturuki na kaskazini mwa Iraq.

Chama cha WaKurd cha PKK hakikutoa idadi ya watu wao waliouawa.

Uturuki piya inawashambulia kwa mabomu wapiganaji wa Islamic State katika maeneo hayo, ili kuleta utulivu katika mipaka yake na Iraq na Syria.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uturuki

Washirika wa Uturuki katika NATO, wameunga mkono haki ya nchi hiyo kujihami, lakini wengine wameeleza wasiwasi, jinsi mashambulio hayo yalivyokuwa makubwa.

Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, ameisihi Uturuki, isivunje kabisa uhusiano iliyojenga na WaKurd walio wachache Uturuki,wanaharakati wa Kikurd wanadai kuwa mashambulio hayo ya Uturuki, yameuwa raia wengi.