Obama alenga sera ya mazingira

Ukame wa California, Marekani Haki miliki ya picha Getty

Rais Obama anasema Jumatatu ofisi yake itatangaza hatua kubwa na muhimu kabisa ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Lengo ni kupunguza gesi inayozidisha joto duniani kwa karibu thuluthi moja katika miaka 15 ijayo.

Kati ya hatua hizo ni kuweka uzito kwenye miradi ya kutumia jua na nishati mbadala nyengine.

Lakini wapinzani katika sekta ya nishati wamelalamika juu ya mpango huo, wakisema kuwa Rais Obama anapiga vita makaa - chanzo cha zaidi ya thuluthi ya mahitaji ya nishati ya Marekani.

Mwandishi wa BBC anasema hatua hizo zinazopendekezwa zitampa rais nguvu ya kujadili mpango wa kupunguza gesi hiyo duniani, kwenye mkutano wa mazingira utaofanywa Paris mwezi wa Disemba.