Wanajeshi 2 wa Uturuki wauawa

Haki miliki ya picha HURRIYET.COM.TR
Image caption Shambulizi la Uturuki

Wanajeshi wawili wa Uturuki wameuawa kwenye shambulizi la bomu katika kituo kimoja cha kijeshi mashariki mwa nchi.

Wanajeshi wengine ishirini na wanne walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo lililotokea katika wilaya ya Dogubayazit wakati wanamgambo waliendesha gari lililokuwa limejazwa vilipuzi na kugonja jengo moja.

Utawala umewalaumu waasi wa kikurdi wa PKK.

Jeshi la Uturuki limekuwa likiendesha mashambulizi ya angani dhidi ya PKK kaskazini mwa Iraq siku za hivi majuzi.