India yazuia mitandao 857 ya ngono

Haki miliki ya picha PA
Image caption Tarakilishi

India imezuia uwezo wa kuingia katika takriban mitandao 857 ya picha za ngono katika kile inachosema ni harakati za kuwazuia watoto kuiona.

Hatahivyo watu wazima wataendelea kuingia katika mitandao hiyo kupitia mitandao ya kibinafsi VPNs.

Mnamo mwezi Julai ,mahakama kuu ilionyesha kutofurahishwa na hatua ya serikali kushindwa kuzuia mitandao hiyo hususan ile ilio na picha za ngono ya watoto.

Kampuni za mawasiliano zimesema kuwa haziwezi kutekeleza marufuku hiyo mara moja.

Image caption Marafuku

''Lazima tufunge kila mtandao mmoja baada ya mwengine na itachukua siku chache kwa wahudumu kuzuia mitandao yote,afisa mmoja wa kampuni hizo za mawasiliano ambaye hakutaka kutajwa aliliambia gazeti la the times kutoka India.

Afisa mkuu ambaye hakutaka jina lake litajwe aliiambia BBC Hindi kwamba idara ya mawasiliano nchini India imeshauri wahudumu wa kampuni hizo kudhibiti mitandao hiyo 857 ya picha za ngono.

Haijapigwa marufuku kabisa,lakini hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na maono ya mahaka kuu kuhusu watoto walivyo na uhuru wa kuingia katika mitandao ya picha za ngono.