Lowassa ndiye mgombea wa CHADEMA

Chama cha upinzani cha CHADEMA nchini Tanzania kimetangaza kuwa aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa atakuwa mgombea wake wa urais wakati wa uchaguzi wa mwezi Octoba.

Bwana Lowassa alijiunga na Chadema wiki moja iliopita baada ya kuhama kutoka chama tawala cha CCM ambapo alikuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 30.

Alifeli katika jaribio lake la kutaka kuwa mgombea wa chama cha CCM mwezi uliopita.