Watu 7 wauawa na wapiganaji Cameroon

Haki miliki ya picha
Image caption Shambulizi Cameroon

Zaidi ya watu 7 wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio linaloaminika kufanywa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram huko kaskazini mwa Cameroon.

Mwandishi mmoja wa habari katika kijiji cha Tchakarmari karibu na mpaka wa Nigeria anasema wanamgambo hao wameshambulia asubuhi na kuteketeza majumba.

Kuna ripoti pia baadhi ya watu wametekwa nyara.

Boko Haram wamekuwa wakiendeleza mashambulio hasa katika nchi jirani na Nigeria wanakotoka licha ya nchi hizo kuunda kikosi cha pamoja cha Nigeria, Cameroon, Chad na Niger kupambana na wanamgambo hao.