Yemen:Waasi wa Houthi wafurushwa kambini

Haki miliki ya picha reuters
Image caption Yemen

Vikosi vinavyounga mkono serikali nchini Yemen vimechukua kambi kubwa ya wanahewa katika makabiliano na waasi wa Houthi ,msemaji wa vikosi hivyo ameambia BBC.

Uharibifu mkubwa pamoja na majeraha yameripotiwa katika kambi ya jeshi ya al-Anad,kaskazini mwa mji wa Aden baada ya mapigano makali yaliofanyika katika siku za hivi karibuni.

Hatua hiyo inajiri baada ya vikosi vinavyounga mkono serikali vikisaidiwa na mshambulizi ya angani ya muungano unaoongozwa na Saudia kuchukua mji wa Aden mwezi Julai.

Raia wa Saudi wanaongoza kampeni ya kuwasukuma waasi hao nyuma na kurejesha serikali wanayoitetea.

Wanajeshi na magari yaliojihami kutoka kwa milki za kiarabu,kiungo muhimu cha muungano huo pia wanadaiwa kuwasili katika siku za hivi majuzi.