UN:Idadi ya vifo Afghanistan imeongezeka

Haki miliki ya picha AP
Image caption UN:Idadi ya vifo ni juu mno Afghanistan

Shirika la Umoja wa mataifa, linasema kuwa ongezeko la idadi ya wanawake na watoto ambao wamejeruhiwa au kuuawa nchini Afghanistan tangu majeshi ya NATO yalipoondoka nchini humo mwezi Disemba mwaka jana, inatisha.

Kupitia ripoti hiyo ya Umoja wa mataifa, idadi ya jumla ya wanawake waliojeruhiwa au kuuwauwa katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, iliongezeka kwa asilimia 23.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bell:katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu,idadi ya vifo vya wanawake iliongezeka kwa asilimia 23

Idadi ya watoto ilipanda kwa silimia 3.

Idadi hiyo imeongezeka kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo, tofauti na milipuko ya mabomu yanayotegwa ardhini.

Sasa shirika hilo la umoja wa mataifa linaomba kundi la wanamgambo wa Taliban na makundi mengine yanayopigana kuliunga mkono taifa hilo kukomesha mashambulio dhidi ya raia.