Mwanajeshi wa Rwanda auwa wenzake CAR

Askari wa usalama mjini Bangui Haki miliki ya picha REUTERS Joe Penney

Wizara ya ulinzi ya Rwanda inasema kuwa mwanajeshi wake mmoja katika kikosi cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati amewapiga risasi na kuwauwa wenzake wane kutoka Rwanda.

Wanyarwanda wengine wanane wamejeruhiwa.

Muuaji naye tena alijiuwa.

Shambulio hilo lilitokea kwenye makao makuu ya kikosi cha Rwanda katika mji mkuu, Bangui.

Msemaji wa jeshi alieleza kuwa pengine chanzo ni ugaidi, lakini amesema ugonjwa wa akili piya unaweza kuwa sababu.