Je washindi wa London Marathon walitumia dawa ?

Haki miliki ya picha BBC0
Image caption Sunday Times:Viwango vyao vya chechembe za damu zilikuwa juu sana

Washindi mara saba wa mbio za masafa marefu ya marathon za London Uingereza walikuwa na matokeo ya kutatanisha baada ya damu yao kupigwa msasa.

Gazeti la Sunday Times la Uingereza limedai kuwa washindi 7 katika kipindi cha miaka 12 walishukiwa kuwa wametumia dawa zilizopigwa marufuku za kuongeza nguvu mwilini.

Gazeti hilo la kila Jumapili linasema kuwa wanariadha 20 ambao walitamba katika mbio hizo walipaswa kuonywa kuhusiana na uwezekano wao kuwa walitumia dawa za kusisimua misuli.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Washindi mara saba wa mbio za masafa marefu ya marathon za London Uingereza walikuwa na matokeo ya kutatanisha baada ya damu yao kupigwa msasa.

Aidha gazeti hilo limedai walipaswa wachunguzwe zaidi ili ukweli ufahamike kutokana na viwango vya juu sana vya chechembe za damu.

Kulingana na jarida hilo, wataalamu wawili waliochunguza takwimu za matokeo ya damu za wanariadha hao wanasema kuwa mashindano ya Marathon ya mji wa London ni mojawapo tu ya

mashindano mengine ya miji 34 ya riadha ambayo matokeo ya uchunguzi wa damu ya washindi wake yaliyotiliwa shaka.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Washindi wa London Marathon walitumia dawa -Sunday Times

Waandalizi wa mashindano hayo maarufu duniani wanasema kuwa wako tayari kutumia njia za kisheria kumpokonya tuzo mshindi wa Marathon aliyepokonywa taji la wanamke

la mwaka 2010, Lilia Shobukhova, baada ya kuthibitishwa kuwa alitumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.