Mpigania Haki za binaadamu Mexico auawa

Image caption Miguel Angel Jimenez Blanco akiagwa na muombolezaji

Mtetezi mmoja wa haki za binaadam nchini Mexico aliyekuwa akizisaidia familia kuwapata ndugu zao waliopotea amekutwa amekufa baada ya kupigwa risasi mwishoni mwa wiki.

Mwili wa Miguel Angel Jimenez Blanco ulikutwa katika taksi moja aliyokuwa akiimiliki karibu na nyumbani kwake (katika mji wa Xaltianguis) Kusini Magharibi mwa jimbo la Guerrero.

Kwa tabia alikuwa na hulka ya kukasirishwa na kile alichokiona kama kutochukua hatua kwa mamlaka husika, Jemenez Blanco alisaidia utafutwaji katika eneo ambalo wanafunzi 43 walipotea karibu na mji wa Iguala mwaka uliopita,pia alifichua upoteaji wa mamia ya watu katika mji huo kunakosababishwa na magenge ya wahuni.