Picha za bomu la nyuklia Nagasaki Japan

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bomu ya kiatomiki ilipolipuka mjini Nagasaki

Huku ulimwengu ukiadhimisha miaka 70 tangu ndege za kijeshi za Marekani ilipodondosha bomu la kinyuklia juu ya Nagasaki tazama picha za janga hilo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Majengo yote na viwanda viliharibiwa kabisa

Ibada maalumu za ukumbusho zinaendelea kufanywa katika mji wa Nagasaki, nchini Japan, kuadhimisha miaka 70 tangu kulipuliwa kwa bomu ya atomiki jijini humo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Zaidi ya watu elfu 70,000 waliangamia
Haki miliki ya picha AP
Image caption Wahasiriwa wa bomu hilo waliungua mwili wao mzima

Tarehe 9 Agosti mwaka wa 1945, ndege ya Marekani ikiwa imejihami kwa silaha zenye nguvu za kitonaradi ilidondosha bomu la pili kuwahi kutupwa katika uwanja wa kivita katika mji wa , Nagasaki ambao ulikuwa ndio kitovu cha uzalishaji wa viwanda nchini Japan.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Siku 6 tu baadaye Japan ilitangaza kuwa imejisalimisha katika vita hivyo vya dunia.

Siku 6 tu baadaye Japan ilitangaza kuwa imejisalimisha katika vita hivyo vya dunia.

Haki miliki ya picha Reuters I Torahiko OgawaNagasaki Atomic Bomb Museum
Image caption Watu 74,000 waliangamia

Takwimu zinasema kuwa takriban watu 74,000 waliangamia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu wengi zaidi walikufa kutokana na athari ya miale ya nyuklia

Hii ilikuwa ni idadi kubwa zaidi ya watu hususan ikitokea siku tatu tu

Image caption Asilimia 70 ya watu hawakuwa na makao

baada ya bomu la kwanza la kinyuklia kuua zaidi ya watu 140,000 mjini Hiroshima.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bomu hiyo iliyotikisa na kuangamiza kabisa mji wa Nagasaki

Bomu hiyo iliyotikisa na kuangamiza kabisa mji wa Nagasaki ilijulikana kwa jina la utani kama ''Fat Man''.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wahasiriwa wa mkasa huo hawataki Japan ijiuhusishe na vita tena

Ndege iliyotumika kutupa bomu hilo ilijulikana kama Bockscar, ilipaa kutoka kisiwa cha Mariana.

Image caption Kanisa kubwa zaidi wakati huo liliharibiwa kabisa

Rubani wake alikuwa Meja jenerali Charles Sweeney.

Image caption Zaidi ya watu 200,000 waliuawa

Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 200,000 waliuawa katika milipuko hiyo miwili,

Image caption Wengine kufariki baadaye kutokana na miale ya sumu kutoka kwa mabomu hayo ya nguvu za kitonaradi

Wengine kufariki baadaye kutokana na miale ya sumu kutoka kwa mabomu hayo ya nguvu za kitonaradi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Viongozi wanamkashifu waziri mkuu bwana Shinzo Abe kwa kubadili sera na katiba ilikuiruhusu nchi hiyo kushiriki kwa vita

Katika ibada ya ukumbusho iliyoandaliwa leo mjini Nagasaki,

Image caption Ndege iliyotumika kutupa bomu hilo ilijulikana kama Bockscar

wahasiriwa walimzomea waziri mkuu wa bwana Shinzo Abe kwa kutaka kubadilisha katiba ya taifa hilo ilikuwaruhusu wanajeshi wa Japan kuhusika na mapigano.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Mnara wa amani umejengwa katika eneo hilo

Meya wa mji wa Nagasaki naye alivutia waya huohuo akimkashifu waziri mkuu bwana Shinzo Abe kwa jitihada za kubadilisha katiba ya nchi.