Watoto wanyanyaswa kijinsia Pakistan

Haki miliki ya picha Getty
Image caption mabango yenye ujumbe wa kutaka uokozi

wanaume saba wamekamatwa mashariki mwa Pakistan wakihusishwa na kashfa za unyanyasaji watoto kijinsia.Waziri mkuu wa jimbo la Punjab,Shahbaz Sharif ameitaka mahakama kutoa hukumu juu ya taarifa zilizotolewa kuhusu watoto mia moja ambao walinyanyaswa kijinsia.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimesema kuwa wahuni hao walitengeneza filamu ya ngono inayoonesha watoto wa kiume wakifanyiwa unyanyasaji wa kijinsia ,huku wazazi wao wakiwa wanatapeliwa.

hata hivyo wiki mbili zilizopita,watu ishirini walijeruhiwa wakati wakiandamana dhidi ya polisi ambaye alimwachia mtuhumiwa wa unyanyasaji wa kijinsia.