Israel yawakamata 7 waliochoma Wapalestina

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Israel yawakamata 7 waliochoma Wapalestina

Maafisa wa Polisi nchini Israeli wamesema kuwa wamewakamata watu 7 wanaoshukiwa kwa kuvamia nyumba moja ya mpalestina katika ukingo wa magharibi na kuiteketeza moto.

Shambulizi hilo lililotokea mwisho wa mwezi uliopita lilisababisha kifo cha mtoto wa mwaka mmoja u nusu.

Shambulizi hilo lililotekelezwa na walowezi wa Kiyahudi lilimuacha bwana Dawabsheh mke wake na mwana wao mwenye umri wa miaka 4 wakiuguza majereha mabaya.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Watu hao wanashukiwa kuwa ndio waliowasha moto ulioua mtoto wa mwaka mmoja u nusu

Hapo jana Mamia ya wakazi wa ukingo wa Magharibi (West Bank) unaokaliwa na Israeli walijitokeza kwa mazishi ya babake mtoto wa kipalestina aliyeteketezwa hadi akafa na walowezi wa kiyahudi.

Sa'ad Dawabsheh aliaga dunia katika hospitali ya Soroka iliyoko Israeli alikokuwa akipokea matibabu baada ya kuungua sehemu kubwa ya mwili wake.

Mke wake bi Riham na mwana wao wa kiume Ahmad bado wako katika hali mahututi hospitalini.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hapo jana Mamia ya wakazi wa ukingo wa Magharibi (West Bank) unaokaliwa na Israeli walijitokeza kwa mazishi ya babake mtoto

Shambulizi hilo lililotokea mwisho wa mwezi Julai liliibua hasira miongoni mwa Wapalestina na wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu ambao waliilaumu Israeli kwa kukosa kuwajibikiausalama wa Wapalestina mikononi mwa Walowezi wa kiyahudi.

Kulingana na ripoti hiyo ya Polisi washukiwa hao walikamatwa katika operesheni iliyofanywa katika makao haramu ya walowezi katika ukingo wa Magharibi.