kumi wauawa nchini Mali

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanajeshi wa nchi ya Mali wakiwa mitaani

Jeshi nchini Mali limesema zaidi ya watu kumi wameuawa katika shambulio moja kwenye mji wa Gaberi kaskazini mwa nchini humo . Shambulizi hili limekuja siku moja baada ya watu kumi na watatu (wakiwemo washambuliaji wanne) kuuawa ambapo washukiwa wa tukio hilo Wanajeshi wa Kiislam walishambuliana na jeshi la serikali walipowazingira kwenye hotel moja katikati mwa mji wa Sevare.

Msemaji wa jeshi la Mali (Souleymane Maiga) alikaririwa akisema ni mapema mno kujua kama mashambulizi hayo mawili yalikua na uhusiano ama la. Watu waishio karibu na Timbuktu wanaamini kuwa shambulio lililotokea Gaberi linaonekana kuwa ni la mgongano wa jumuiya. Hakuna kundi lolote lililothobitisha kufanya mashambulizi hayo.