Watoto 70 waliofungwa waokolewa Cameroon

Image caption Cameroon

Polisi waliojihami nchini Cameroon wameivamia nyumba moja na kuwaokoa watoto wapatao 70 waliokuwa wamefungwa.

Miongoni mwao ni watoto waliofungwa kwa minyororo kwa miaka mitatu.

Nyumba hiyo ipo katika mtaa wa Ngaoundere, kaskazini mwa nchi hiyo.

Inaarifiwa inamilikiwa na mwalimu wa shule ya kufunza Quran.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari kutoka eneo hilo, amesema wazazi wa watoto hao waliwapeleka kwa hiari watoto wote kwenye kituo hicho anachokitaja kuwa cha kufunza adabu.

Wengi wao waanarifiwa kuwa katika hali mbaya.