Weusi 2 wapigwa risasi Ferguson,Marekani

Haki miliki ya picha Sid Hastings l EPA
Image caption Watu 2 weusi walipigwa risasi na polisi katika maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa mvulana mweusi huko Ferguson, Missouri

Mtu mmoja amejeruhiwa vibaya huko Ferguson, Missouri, huko Marekani baada ya kisa cha ufyatulianaji risasi uliotokea katika dakika za mwisho mwisho za maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuuawa kwa mvulana mweusi Michael Brown na polisi mwaka uliopita.

Kisa hicho cha mauaji kilisababisha mtafaruk baina ya watu wa jamii ya wamarekani weusi na polisi.

Barubaru huyo tayari amefanyiwa upasuaji na anasemekana hali yake ya afya imedhibitiwa kwa mujibu wa polisi.

Polisi wanasema kuwa walikuwa wakimsaka barubaru huyo kwa kipindi kirefu baada ya kupokea habari kuwa alikuwa amejihami kwa bunduki iliyoibwa.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Taharuki imetanda Ferguson, Missouri baada ya video kuibuka ikionesha polisi wakimpiga risasi mtu mweusi

Jina la mhasiriwa huyo halijajulikana kufikia sasa.

Mkuu wa polisi katika jimbo hilo la Ferguson Jon Belmar amesema kuwa tayari maafisa 4 wa polisi wamehssimamishwa kazi ilikufanikisha uchunguzi wa kina kuhusu kisa hicho.

Picha kutoka eneo la tukio zinaonesha mtu mweusi anayetokwa na damu akiwa amelala sakafuni.

Awali,mamia ya watu walisimama kimya kwa muda wa dakika nne na nusu kwa pamoja mjini Ferguson ,Missouri katika sehemu ile ile ambayo kijana asiye na hatia Michael Brown aliuwawa na polisi mmoja wa kizungu mwaka mmoja uliopita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tukio hilo lilitokea baada ya maandamano ya kuadhimisha mauji ya Michael Brown na polisi mzungu

Ishara hiyo inaashiria muda ambao mwili wake ulilala katikati ya barabara bila kupata msaada wowote.

Njiwa wawili walipeperushwa hewani na watu waliandamana kimya kimya ili kutoa heshima kwa Michael Brown na wengine ambao walikufa katika mikono ya polisi.

Mauaji hayo yalileta mjadala dhidi ya ubaguzi wa polisi nchini Marekani na ulimwenguni.