Furguson:kijana ajeruhiwa na kukamatwa

Image caption Hamkani si shwari Ferguson

Hali ya tahadhari imetangazwa katika mji wa Marekani Ferguson. Mvutano ulienea baada ya kijana mweusi wa miaka kumi na nane kujeruhiwa kwa risasi na polisi mwishoni mwa maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Waendesha mashitaka wametamka kuwepo kwa hatia kwa kijana Tyrone Harris ambaye yu mahututi hospitalini.Kijana huyo alikua akishiriki katika maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja tokea kifo cha rafiki yake Michael Brown, kijana mweusi aliyeuawa na polisi mzungu mwaka wa jana ambaye baadaye ilisemekana hakuwa na hatia.

Polisi walisema Tyrone Harris alikuwa miongoni mwa watu sita ambao waliwafyatulia risasi maafisa. Baba yake anasema mwanaye hakua na silaha na alijaribu kukimbia kujihami.