Maafisa tisini wazuiliwa Cuba

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Kerry ,waziri wa mambo ya nje wa Marekani

Serikali ya Marekani imesema ina wasiwasi mkubwa kuhusiana na kuzuiwa kwa wapinzani tisini katika mji mkuu wa Cuba, Havana mwishoni mwa wiki.

Wajumbe wa kundi moja la kipinzani la wasichana wanaovaa nguo nyeupe walisema kuwa wanausalama wa Cuba waliwazingira na kuwashililia kisha kuwaachilia huru baada ya saa manne unusu.

Kukamatwa huko kumekuja siku chache kabla ya ziara ya John Kerry jijini Havana, ziara ambayo ni ya kwanza kutoka kwa kiongozi wa marekani baada ya miaka saba.

Kerry atahudhuria uzinduzi wa ubalozi wa Marekani nchini Cuba.Nchi zote mbili zilifungua tena balozi zake katika miji mikuu ya nchi zao mnamo mwezi january mwaka huu. Taasisi ya kutetea haki za binaadam nchini Cuba wamesema wapinzani nchini humo wamekua wakisumbuliwa mara kwa mara na kumekuwako vizuizi vya muda zaidi ya mia sita na sabini na nne tangu juni 2014.