UK yapinga kesi ya mpelelezi mkuu Rwanda

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Jenerali Karenzi Karake

Mahakama ya Uingereza imekataa mpango wa kumsafirisha hadi nchini Uhispania afisa mkuu wa idara ya upelelezi wa Rwanda ili ashtakiwe na jukumu alilochukua wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Karenzi Karake alikuwa amewachiliwa kwa dhamana nchini Uingereza kufuatia kukamatwa kwake mnamo mwezi Juni na kibali kilichotolewa na uhispania.

Kukamatwa kwake kuliathiri hali ya kidiplomasia kati ya Uingerewza na Rwanda.Jaji wa Uhispania alimshtaki Jenerali Karake mwaka 2008 kwa madai ya uhalifu.

Uamuzi huo wa Uingereza umeungwa mkono na waziri wa haki nchini Rwanda Johnston Busingye.