Ubalozi wa Marekani washambuliwa Uturuki

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Shambulizi nchini Uturuki

Watu wenye silaha wameufyatulia risasi ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Uturuki, Istanbul.

Watu wawili walitoroka wakati maafisa wa polisi walipowafyatulia risasi lakini ripoti zinasema kuwa mshukiwa mwanamke tayari ametiwa mbaroni.

Hakuna habari zo zote za majeruhi zilizotolewa.

Shambulio hilo lilitokea muda mfupi baada ya bomu kulipuka kwenye gari moja lililokuwa limeegeshwa karibu na kituo cha polisi.

Watu kumi walijeruhiwa, wakiwemo maafisa watano wa polisi.

Inasemekana kuwa washukiwa wawili na afisa mmoja wa polisi walifariki.

Haijulikani iwapo mashambulizi hayo mawili yana uhusiano.

Uturuki imewekwa katika hali ya tahadhari tangu ianzishe mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State wa Syria na Wakurdi Kaskazini mwa Iraq.