PKK:Uturuki inawatetea Islamic State

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kambi ya PKK

Mtu anayeongoza chama cha Wafanyikazi wa Kurdistan PKK ameishtumu Uturuki kwa kujaribu kuwatetea wapiganaji wa Islamic state kupitia kuwashambulia wapiganaji wa kikurdi.

Cemil Bayik ameiambia BBC kwamba anaamini rais Recep Tayyip Erdogan anataka wapiganaji wa Islamic state kufanikiwa kwa lengo la kuzuia ufanisi uliotekelezwa na wapiganaji hao.

Wapiganaji wa Kikurdi wakiwemo wale wa PKK wamepata mafanikio makubwa dhidi ya wapiganaji wa Islamic State nchini Syria na Iraq.

Lakini Uturuki,kama mataifa mengine ya magharibi yanaliona kundi hilo kama la kigadi.

Makubaliano ya kusitisha vita na kundi hilo yalisambaratika mwezi Julai,wakati Uturuki ilipoanza kuzilipua kambi za PKK kaskazini mwa Iraq,mbali na kuwashambulia wapiganaji wa Islamic state.

Waangalizi wanasema kuwa wapiganaji wa PKK wamekuwa wakishambuliwa zaidi ikilinganishwa na IS.