UN yapeleka maafisa wake nchini Burundi

Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa Burundi,Pierre Nkurunziza

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeunga mkono mpango wa kutuma maafisa wake wa ngazi ya juu nchini Burundi kwa ajili ya kutatua hali ya sintofahamu iliyopo nchini humo.

Baraza la hivi sasa lililopo chini ya Mnigeria Joy Ogwu limesema kuwa kumekuwepo na wasiwasi mkubwa juu ya hali ya usalama nchini Burundi huku likitoa wito kwa serikali kufanya mazungumzo ya amani na upande wa upinzani.

Kiongozi mwandamizi wa umoja wa mataifa kuhusiana na haki za binaadam Ivan Simonovic, ambaye alipelekwa na baraza hilo alisema hali ilikua ya kuzorota nchini Burundi lakini bado hawajakata tamaa.

Tangu,Rais Pierre Nkurunzinza , mapema mwaka huu kutangaza azma yake ya kugombea awamu ya tatu ya kuitawala nchi hiyo hali ya usalama bado haijatengamaa.