Afrika yaadhimisha mwaka mmoja bila Polio

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Polio

Afrika imepiga hatua kubwa katika kuangamiza ugonjwa wa kupooza Polio.

Bara hili linaadhimisha mwaka mmoja tangu kisa cha mwisho kiripotiwe katika mtoto mdogo nchini Somalia.

Huku wataalam wa afya wakifurahishwa na hatua zilizopigwa Shirika la afya duniani limeonya dhidi ya kulegeza msimamo .

Linasema kuwa chanjo dhidi ya watoto inapaswa kuendelea kutolewa ,lakini swala la usalama nchini Somalia na Nigeria linatoa changamoto chungunzima.

Bara la Afrika linatarajiwa kutoripoti visa vyovyote vya ugonjwa huo kwa miaka miwili zaidi kabla ya ugonjwa huo kuripotiwa kuangamizwa barani humo.