Japan yafufua kiwanda chake cha nyuklia

Haki miliki ya picha
Image caption Raia wapinga kuanzishwa upya kwa kiwanda hicho

Japan imefufua mojawapo ya viwanda vyake vya kutengeneza umeme wa kutumia nyukilia, miaka minne tangu kuvuja kwa sumu kutoka kwa kiwanda chake kimoja cha kule fukushima .

Kiwanda hicho kilichoko Sendai kilipewa idhini kuendesha shughuli zake Kusini mwa Japan baada ya kupigwa msasa kikamilifu na kuwekewa masharti magumu.

Hata ingawa makundi mbalimbali nchini yanapinga kuanzishwa upya shughuli za kuzalisha umeme kutoka kwa nyukilia, watengenezaji wa umeme kote nchini wametuma maombi kufufuliwa upya vinu 25 vya umeme wa nyukilia.

Mtengenezaji wa umeme katika Sendai ametumia jumla ya dola milioni 20 kukarabati kinu chake.