Mazungumzo ya amani kuhusu Libya yaanza

Haki miliki ya picha Getty
Image caption mazungumzo ya Libya

Mazungumzo kuhusu Libya yalioidhinishwa na Umoja wa mataifa yameanza huko Geneva leo yanayonuiwa kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Tangu kupinduliwa kwa kanali Muammar Gaddafi miaka minne iliyopita , libya imeingia vitani na kumeshuhudiwa ukosefu wa sheria na nchi hiyo sasa ina serikali mbili pinzani, zote zikidai kuwa halali.

Haijakuwa rahisi kwa Umoja wa mataifa kuzishawishi pande mbili pinzani Libya kuhudhuria mazungumzo haya.

Lakini wametuma wawakilishi wao Geneva.

Huenda mwishowe wasikutane ana kwa ana lakini hata hivyo mazungumzo hayo na wanadiplomasia wa Umoja huo huenda yakafanikiwa kuhusu namna ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Na huenda Umoja huo usingeandaa mkutano huu iwapo maafisa wa makundi hayo wangekuwa hawana maatarajio kuwa yataisadia hali.

Tatizo ni kwamba makundi ya kisiasa Libya yamepoteza ushawishi kwa makundi yaliojihami kwa hivyo hata makubaliano yakiafikiwa, huenda yasisaidie kusitisha ghasia.