Wapiganaji wa Kikurdi washambuliwa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Makabiliano kati ya wanajeshi wa Uturuki na wapiganaji wa PKK

Uturuki imeanzisha tena msururu wa mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi yanayolenga maeneo 17 kusini mashariki, kwa mujibu wa jeshi

Maeneo hayo yapo mkoani Hakkari katika mpaka na Iran pamoja na Iraq.

Uturuki imushuhudia ghasia zaidi katika wiki za hivi karibuni kati ya wanajeshi na wapiganaji wa Kikurdi wanaotaka kujiondoa.

Mashambulio hayo yanajiri siku moja baada ya watu tisa kuuawa katika msururu wa mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama, wengine wakiwa katika eneo la kusini mashariki.

Mashambulizi ya jumatatu yanalaumiwa kutekelezwa na kundi la wakurdi la PKK.