India yaishtaki kampuni ya Nestle

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maggy Noodles

Serikali ya India inaishtaki kampuni ya Nestle kwa malipo ya dola milioni 100 kwa mfumo wa biashara usio halali kulingana na afisa mmoja.

Malalamishi hayo dhidi ya kampuni ya Nestle ni kwamba ilifanya uharibifu kwa watumiaji kupitia uongo katika matangazo yake kuhusu bidhaa ya tambi za Maggi noodles.

Tambi hizo za maggi Noodles zilipigwa marufuku nchini India baada ya idara inayosimamia usalama wa bidhaa za vyakula kuishtumu Nestle kwa kushindwa kuafikia viwango vya chakula vilivyo salama.

Hatahivyo Nestle imekana hilo na kusema kwamba bidhaa zake ziko salama katika mahakama ya Bombay.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maggy noodles

Lakini kampuni hiyo ambayo inadhibiti asilimia 80 ya soko la tambi za maggi noodles tayari imeharibu tani 400 za bidhaa za maggi.

Madai hayo yaliowasilishwa kwa niaba ya watumiaji wa India hayakuwasilishwa kupitia mahakamani bali kupitia tume ya kitaifa ya watumiaji ya kutatua mizozo ambayo ina nguvu karibu na zile za mahakama.