Marikana:Familia zaishtaki serikali

Image caption Marikana

Familia za wachimbaji mgodi 37 waliouawa na polisi nchini Afrika Kusini wakati wa mgomo mnamo 2012 wamewasilisha kesi dhidi ya serikali.

Jamaa hao wanadai malipo kwa kupoteza kipato, na gharama za hospitali kutokana na mshtuko wa kiakili na kihisia.

Wanataka pia waziri wa idara ya polisi aombe msamaha rasmi kwa kuwapoteza jamaa zao waliokuwa wakifanya kazi katika mgodi wa madini ya Platinum wa Marikana katika jimbo lililopo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marikana.

Ripoti iliyosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu mauji hayo iliyotolewa Juni iliwalaumu kwa pamoja wamiliki mgodi huo Lonmin maafisa wa polisi pamoja na vyama vya wafanyakazi kwa mauaji hayo.