Askofu ataka majadiliano kuhusu B Haram

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram

Katibu Mkuu wa kanisa la Anglicana duniani Askofu Mkuu Josia Idowu Fearon amewataka viongozi wa dini ya kikristo nchini Nigeria kufanya kazi kwa karibu na waislamu ili kupambana na tishio la Boko Haram nchini humo.

Askofu huyo ambaye anatoka katika eneo la kaskazini mwa Nigeria ndio katibu mkuu mpya wa kanisa Anglikana ambalo linawashirikisha waumini milioni 85 kote duniani.

Katika mahojiano na BBC amesema kuwa juhudi zake za kuunga mkono mazungumzo kati ya wakristo na waislamu nchini Nigeria yamekandamizwa na wanachama wa kanisa la Nigeria ambao wanahofu kwamba taifa hilo linabadilishwa na kuwa la kiislamu.

Mnamo mwezi Aprili kanisa la Nigeria lilitoa taarifa likijitenga na uteuzi wa Askofu Idowu kwa kuwa alipinga watu wanaowachukulia kama wahalifu wapenzi wa jinsia moja.