Uamuzi wa Uturuki watiliwa shaka na US

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uturuki

Marekani imetilia shaka uamuzi wa Uturuki wa kutaka kutenga eneo la amani la kutumiwa na raia Kaskazini mwa Syria kwa msaada wa Marekani na mataifa mengine washirika.

Msemaji wa mashauri ya nje wa Marekani, Mark Toner, alisema kuwa msaada wa Marekani utalenga kuwatimua wapiganaji wa Islamic State kutoka eneo hilo kwa ujumla.

Awali waziri mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, alisema kuwa taifa lake linatarajia kwamba litasaidiwa na mataifa ya Magharibi kutenga eneo la amani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa wa polisi wa Uturuki

Aliambia BBC kwamba wanajeshi wa mrengo wa kadri watatoa usalama kwa raia katika eneo hilo dhidi ya wanajeshi walio waaminifu kwa Rais Assad.