Watu 60 wameuawa Baghdad

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu 30 wameuawa Baghdad kufuatia bomu kubwa lililotegwa ndani ya lori

Mlipuko mkubwa kutoka kwa lori lililokuwa limeegezwa katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad umesababisha vifo vya zaidi ya watu 60.

Maafisa walisema kuwa gari lililokuwa na mtambo wa kutengeneza barafu lililipuka Kaskazini Mashariki mwa jiji hilo.

Mlipuko huo ulitokea katika eneo la soko lililo na watu wengi karibu na Wilaya inayokaliwa zaidi ya Washia ya Sadri.

Haki miliki ya picha .
Image caption Hakuna kundi lolote lilolodai kuhusiana na mlipuko huo.

Hakuna kundi lolote lilolodai kuhusiana na mlipuko huo.

Wapiganaji wa kundi la Waislamu wenye itikadi kali hushambulia maeneo yanayokaliwa na Washia mara nyingi.