CNN yaiomba Kenya radhi kwa ripoti potofu

Image caption ''CNN wameomba msamaha kwa ripoti yao ya uongo'' Kenyatta

Baada ya malumbano makali kati ya wa-Kenya na shirika la habari la habari la kimataifa la CNN,limeomba radhi Kenya kuhusiana na taarifa iliyopeperushwa hewani,ikidai kuwa Kenya ni kitovu cha ugaidi.

Mkurugenzi mkuu, wa CNN Tony Maddox alizuru Nairobi hiyo jana na kukutana na uongozi wa Kenya na kuomba radhi.

Rais Uhuru Kenyatta kupitia mtandao wake wa Twitter alisema kuwa Bwana Maddox ameomba radhi kibinafsi.

Rais Kenyatta alisema kuwa Maddox alikiri kuwa Mwandishi wa habari hiyo alikosea.

'Kwa kweli Kenya sio kitovu cha ugaidi'' alisema Maddox

Image caption Kenyatta 'CNN wamekiri kuwa ripoti hiyo haikuwa ya kweli'

Wakenya mara moja walimrukia bwana Maddok kwa kibwagizo #uhurutellCNN

''Mtembeze huyo mtu katika mbuga zetu ilimwenyewe ajione kuwa sisi ni kitovu cha ubunifu''

''Wengine walimtaka rais Kenyatta amruhu atembelee vitongoji vya kifahari ambapo mali nyumba na unadhifu unazidi ule wa Marekani''

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption 'Kwa kweli Kenya sio kitovu cha ugaidi'' alisema Maddox

Rais Kenyatta alijibu kwa niaba ya wakenya ''Bwana madox je umeshuhudia ugaidi ?

Hiyo ndio sababu wakenya walikasirishwa sana na ripoti hiyo potofu.

Kwa hakika hakuna sababu ya CNN kupeperusha ripoti hiyo kwa lengo la kuichafulia jina Kenya ilihali taifa lilikuwa linajiandaa kumwalika mwana wao ambaye ni rais wa Marekani Barack Obama.''

Hata hivyo wachanganuzi wa maswala ya ndani ya habari, wanasema kuwa huenda mkurugenzi mkuu wa CNN aliogopa kupoteza kandarasi ya matangazo kutoka Kenya yenye thamani ya mamilioni ya dola.

Kenya hunadi utalii wake kupitia shirika hilo la habari kwa gharama ya zaidi dola milioni mia moja.

Punde baada ya tangazo hilo lililoudhi sana serikali ya Kenya ,yamkini Kenya ilipiga marufuku kandarasi hiyo.

Ripoti hiyo vilevile inafwatia ile ya mwaka wa 2013 ambayo ilisema kuwa kuna uwezekano wa kutibuka machafuko kama yale yaliyotokea mwaka wa 2007.

Haki miliki ya picha
Image caption CNN yaiomba Kenya radhi kwa ripoti potofu

Ripoti hiyo iliyochapishwa kabla ya uchaguzi mkuu wa Kenya ilidai kuwa watu wameanza kujihami tayari kwa mapigano mapya.

Ripoti hiyo ilipatikana kuwa uongo.