Operesheni kali kukomboa Sirte Libya

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Operesheni kali kukomboa Sirte Libya

Wizara ya ulinzi mjini Tripoli, ambao ulitwaliwa na na kundi la wanamgambo wa kiislamu lijulikanalo kama Fajir, ilitoa taarifa ikisema kuwa operesheni kali imeanzishwa ili kukomboa mji wa sirte.

Taarifa hiyo imesema kuwa operesheni hiyo inaongozwa na kundi la vijana na wakaazi wa eneo hilo la sirte na wapiganaji wengine ambao wamejitolea.

Kufuatia kuondolewa madarakani kwa Muammar Gadafi mwaka wa 2011, Libya imekuwa na mabunge mawili na serikali mbili ambazo zimekuwa ziking'ang'ania madaraka moja ikiwa na makao yake mjini Tripoli na nyingine ikiwa mjini Tobruk mashariki mwa nchi hiyo.

Image caption Serikali iliyo na makao yake mjini Tobruk ndio inayotambuliwa na jamii ya kimataifa.

Serikali iliyo na makao yake mjini Tobruk ndio inayotambuliwa na jamii ya kimataifa.

Kundi la Islamic State ambalo linathibiti eneo kubwa nchini Iraq na Syria, limetumia mgogoro wa kisiasa nchini Libya kuimarisha ushawishi wake hasa ilipouteka mji wa sirte ulioko takriban kilomita 450 mashariki mwa mji mkuu wa tripoli.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Libya imekuwa na mabunge mawili na serikali mbili ambazo zimekuwa ziking'ang'ania madaraka

Serikali ya Tobruk imelaani machafuko yanayoendelea mjini Sirte na kutoa wito kwa jamii ya Kimataifa kuwajibika na kutekeleza majukumu yake dhidi ya kundi hilo la Islamic State.

Taarifa hiyo imesema kuwa jamii ya kimataifa hasa nchi zenye ushawishi mkubwa zinatumia rasilimali nyingi kupambana na kundi hilo la IS nchini Syria na Iraq lakini imeifumbia macho tatizo la kuwepo kwa wapiganaji wa kundi hilo nchini Libya.